0


Liverpool imewashinda kirahisi mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza Leicester katika mchezo wao wa kwanza wakichezea katika dimba la nyumbani katika msimu huu.

Wekundu hao walionekana hawakamatiki baada ya Roberto Firmino kuunganisha pande la James Milner na kuandika goli la kwanza, kicha Daniel Sturridge kutoa pasi ya kisigino iliyofungwa na Sadio Mane.

Hata hivyo Leicester ilifufua matumaini pale pasi safi ya Lucas kunaswa na mshambuliaji wao machachari Jamie Vardy na kutikisa nyavu. Hata hivyo Adam Lallana akaongeza lingine na kisha Firmino kufunga la nne kufuatia pasi ya Mane.

Roberto Firmino  akitoka nduki kushangilia goli lake alilofunga

Jamie Vardy akiokota mpira wavuni baada ya kufunga goli pekee la Leicester City

Post a Comment

 
Top