
Ilimchukua dakika sita tu Cristiano Ronaldo kufunga goli lake la kwanza akirejea dimbani kwa mara ya kwanza katika msimu huu na kuisaidia Real Madrid kuibuka na ushindi mnono wa magoli 5-2 dhidi ya Osasuna.
Cristiano Ronaldo, aliyerejea dimbani baada ya kuumia goti lake katika mchezo wa fainali ya Euro 2016 dhidi ya Ufaransa, aliunganisha wavuni mpira wa krosi uliopigwa na Gareth Bale.
Danilo alifunga goli la pili. Sergio Ramos na Pepe walifunga kwa kichwa mipira ya kona ya Toni Kroos na Luka Modric kufunga la tano, kabla ya Oriol Riera na David Garcia kuchomoa mawili.

Cristiano Ronaldo akiunganisha wavuni krosi ya Gareth Bale

Cristiano Ronaldo akimkimbilia Gareth Bale kumpongeza kwa kumpasia pande lililoza goli
Post a Comment