
Mabingwa watetezi wa ligi ya La Liga Barcelonawamepata kipigo kutoka kwa timu iliyopanda daraja ya Alaves wakati kocha Luis Enrique aliposhusha kikosi chake akiwaacha benchi nyota wake Lionel Messi na Luis Suarez.
Katika mchezo huo mshambuliaji Mbrazili Deyverson aliwanyamazisha mashabiki wa Barcelona katika dimba la Nou Camp alipounganisha wavuni mpira wa krosi kutoka kwa Kiko Femenia kwa umbali wa yadi saba.
Beki Jeremy Mathieu aliisawazishia Barcelona kufuatia kona iliyopigwa na Neymar aliyetokea benchi, hata hivyo Ibai Gomez aliifungia Alaves goli la ushindi na kufanya matokeo kuwa Alaves 2- 1 Barcelona.

Deyverson akishangilia goli lake aliloitungua Barcelona

Beki Jeremy Mathieu akifunga kwa kichwa goli pekee la Barcelona
Post a Comment