0













Mchezaji Alexandre Pato amepachika bao akiichezea kwa mara ya kwanza Chelsea huku Aston Villa ikiendelea kushuka chini kuelekea timu zenye kuweza kushuka daraja, baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-0.

Katika mchezo huo wenyeji Aston Villa walijikuta wakizomewa wao pamoja na mmiliki wao Randy Lerner, wakati Chelsea ikitawala kipindi cha pili. Mabao ya Chelsea yalifungwa na Loftus-Cheek, Pato na Pedro aliyrfunga mawili.


Pato ambaye alichukuliwa kwa mkopo kutoka Corinthians akipiga bao la mkwaju wa penati

Post a Comment

 
Top