0














Goli la dakika ya 85 la Cristiano Ronaldo limeipatia Real Madrid ushindi ikiwa imebakia na wachezaji 10, na kumaliza rekodi ya Barcelona kushinda michezo 39 bila ya kufungwa katika Ligi ya Hispania, La Liga.

Katika mchezo huo Barcelona ilikuwa ya kwanza kupachika bao katika dakika ya 56 kupitia kwa Gerard Pique aliyepiga kichwa cha nguvu na kutinga wavuni, hata hivyo Karim Benzema alisawazisha kwa bao safi kabla ya Ronaldo kufunga la pili na matokeo kuwa 2-1.

Katika matokeo mengine ya mechi za La Liga hapo jana ni kama ifuatavyo:- Atl Madrid 5-1 Real Betis, Las Palmas 2-1 Valencia na Celta de Vigo 1-1 Deportivo.


 Karim Benzema akifunga bao la kusawazisha


Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo

Post a Comment

 
Top