
Bondia Callum Smith alihitaji chini ya dakika mbili tu kuweza kupata ushindi mzuri dhidi ya Hadillah Mohoumadi katika pambano la taji la Ulaya la super-middleweight katika ukumbi wa Echo Arena, Jijini Liverpool.
Mfaransa Mohoumadi aliingia ulingoni kwa manjonjo ya kurukaruka na kuyumba lakini mpinzania wake alimnasa na kumbana kwenye kamba za ulingo huku akimtupia makonde hadi refa akasitisha pambano.
Pambano hilo lililoisha ndani ya dakika moja na sekunde 41, limemfanya Smith kuweka rekodi ya kushinda mapambano 19 yote aliyocheza na kujiweka kwenye nafasi ya kuwania mkanda wa dunia wa uzito huo.

Bondia Smith akimshindilia ngumi Halilah Mohoumadi

Ngumi ya kushoto ya Smith ikimuingia barabara Halilah Mohoumadi

Basi utaua: Refa akiingia kati kusitisha pambano hilo baada ya Mohoumadi kuzidiwa kwa kipigo
Post a Comment