0


















Mtu anayeendesha mauaji wa mfululizo katika Mji wa Nakuru nchini Kenya, yanayowalenga wanawake wanaojiuza miili yao bado hajapatikana kwa miezi mitatu, ambapo wanawake saba wanaojiuza wameshauwawa tangu Oktoba mwaka jana hadi Januari hii.

Maafisa polisi wanaochunguza mauaji hayo walimkamata mwanamke mmoja Januari 13 na kumshikilia kwa siku mbili na kumuachia, na jumatatu ya Januari 18 polisi walimkamata mwanaume mmoja kwa kuhusika na mauaji hayo ambaye bado anashikiliwa.

Hii si mara ya kwanza Kenya kutokea uhalifu wa muaji ya mfululizo yanayowalenga wanawake wanaojiuza miili yao. Mwaka 2010 mtuhumiwa Philip Onyancha alikiri mahakamani kuwa aliwauwa watu 19, wengi wao wakiwa ni makahaba na kisha kunywa damu zao.


Onyancha aliyefanya mauaji hayo kwa muda wa mwaka mmoja, alitiwa hatiani na mahakama na kuhukumiwa kifungo cha miaka 12 jela.





Post a Comment

 
Top