
Mchezaji aliyetokea benchi Charlie Austin amefunga bao ndani ya dakika saba akiichezea kwa mara ya kwanza Southampton na kupelekea wachezaji wa Manchester United watoke dimbani wakizomewa na mashabiki wao baada ya kulala kwa bao moja kwa bila.
Austin aliruka juu na kupiga mpira wa kichwa uliozaa goli akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa katika dakika ya 87, na kuifanya Southampton kuibuka na ushindi huo kwenye dimba la Old Trafford, katika mchezo huo uliokuwa na nafasi chacheza kufunga.
Post a Comment