Mbunge wa jimbo la Bumula nchini Kenya Bw. Boniface Otsiula ametoa kali ya mwaka baada ya kuwataka wanawake katika jimbo lake kujifungua watoto wengi wawezavyo ili kulijaza jimbo hilo.
Mbunge Otsiula amesema jimbo hilo linaidadi ndogo ya watu, kutokana na ukweli kuwa wanawake wengi wanatumia njia za mpango wa uzazi zinazowafanya washindwe kuzaa na kuongeza idadi ya wapigakura ambayo ni ndogo kwa sasa.
Akiongea kwenye shule ya Sekondari ya Ng'oli mwishoni mwa wiki, Bw. Otsiula mesema jimbo hilo linahitaji kuwa na watoto wengi, ambao watakapokuwa watakuwa wapigakura badala ya kuwauwa kwa mbinu za mpango wa uzazi.


Post a Comment