
Theluji kubwa iliyofunika mashariki mwa Marekani imewafanya wakazi wa majiji ya New York na Washington DC wanaofikia milioni 85 kukwama kufanya shughuli zao za kila siku.
Theluji hiyo inafikia upana na sentimita 102 katika baadhi ya maeneo, imefanya huduma za usafiri wa reli na ndege kukwama, huku umeme ukikatika kwa watu wapatao 200,000.
Amri ya kutosafiri iliyowekwa Jijini New York lililoshuhudia theluji kubwa iliyoshuka na kuweka rekodi, inatarajiwa kuondolewa baadae leo.
Post a Comment