Mshambuliaji wa Leicester City Riyad Mahrez ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika inayotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Mchezaji huyo raia wa Algeria ambaye aliisaidia Leicester kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza, pia ni mchezaji bora wakulipwa wa Afrika na Mchezaji Bora wa Mwaka wa BBC
Katika tuzo hizo mchezaji wa Borussia Dortmund, raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang alishika nafasi ya pili na mshambuliaji wa Liverpool Msenegal Sadio Mane wa tatu.
Mchezaji wa Arsenal raia wa Nigeria mshambuliaji Alex Iwobi ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kijana.
Mchezaji wa Arsenal Alex Iwobi
Post a Comment