![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgbqbVudOMnsLcfuCLIF2q9qd98OrxZlxfRmJfacGfjgKCfk5_GdN76bSMkh9lE0brdgHmgh-VWAJVTZ6wi2CAjeC4J3EwCdsCm164LE51Twa5i-pF5QRNLPfF9W4-R3SHYGFGDLOM4FDw/s640/B.jpg)
Athletic Bilbao imepata ushindi katika mzunguko wa kwanza wa 16 bora katika kombe la Copa del Rey kwa kuifunga Barcelona magoli 2-1 licha ya kumaliza mchezo huo wakiwa na wachezaji tisa.
Katika mchezo huo magoli mawili yaliyofungwa katika dakika tatu na Aritz Aduriz na Inaki Williams yaliwafanya wenyeji Bilbao kuutawala mchezo huo dhidi ya wageni Barcelona.
Mshambuliaji nyota wa Barcelona Lionel Messi alifunga goli la kufutia machozi katika kipindi cha pili kwa mpira wa adhabu, kisha baadaye akakosa goli katika dakika za majeruhi baada ya mpira kugonga mwamba. Raul Garcia na Ander Iturraspe walionyeshwa kadi nyekundu.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiEkA2aqUUP-bki9g_YJFBOWpzbDZFQSjGipwCreGTvvyKagKFHplahRvNl1maYcp5QlreLWhgTimZKXBzNAlYZdg1uKJdaYM7hRZuLzS0F1V_Z2fvzRaWTpZOG5Tgz4Q5uMPqghlzKRoE/s640/B1.jpg)
Aritz Aduriz akifunga goli la kwanza kwa mpira wa kichwa
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi9CYp0lTWqOCBpQeXGPYX4lpBjsPM8OnhuPHZX_z9rsv3Hditx6iVIl6raQMVew4bU-hvw0P0PsjCU7ycABDIRTRadTE67OWi4zufaU9HhOBeOhyphenhyphenMhvG1Wn6zQDDAD-mC3WNYYJ14mSeM/s640/B2.jpg)
Inaki Williams akiwa ameachia shuti lililoandika goli la pili
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgj0_KmYx76OsPDPNJh6_sCMBSwX7pC-2P0zEQWEmJgu0a1vd4JU__0PkCdFHW_XlQ484iPifECFcQrLqAZJhwAp7ur1WyVyqzvPG8bB_hRlFJF0FV3Ue0CgL49lyj_4LiZ8thw1p9f8e8/s640/B3.jpg)
Lionel Messi akishangilia goli la kufutia machozi alilofunga
Post a Comment