
Alexandre Lacazette amekuwa mchezaji wa Arsenal, aliyeweka rekodi katika klabu hiyo kwa uhamisho wa paundi milioni 53 akitokea Lyon ya Ufaransa.
Mchezaji huyo Mfaransa alikuwa katika mazoezi ya Arsenal juzi na kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kukamilisha uhamisho rasmi.
Na jana mchana makubaliano ya uhamisho yalikamilika, ambapo Lacazette alitia saini mkataba wa miaka mitano kuitumikia Arsenal.

Alexandre Lacazette akiwa na kocha wa Arsene Wenger baada ya kusaini mkataba
Post a Comment