0

Wafanyakazi wa kampuni ya Google huenda ni kati ya wafanyakazi wenye mazingira bora na ya matanuzi kazini kutokana na kuwa na bwawa la kuogelea, viwanja vya michezo kama gofu, sauna pamoja na vitanda vya kulala kwa muda.

Wafanyakazi wa kampuni hiyo kubwa ya teknolojia pia hupatiwa chakula cha bure, hukatwa nyweli kwenye saluni ya ofisi na kuruhusiwa kuja na mifugo kama vile mbwa na paka, hata hivyo wafanyakazi wote wanakatazwa kunenepa.


Katika makao makuu ya Google yanayojengwa Jijini London yatakayotumika na wafanyakazi 7,000 yanatarajiwa kuwa na eneo la kukimbilia, kiwanja cha mpira wa kikapu pamoja na chumba cha kufanyia masaji.

 Mmoja wa wafanyakazi wa kike wa Google akicheza gofu ofisini


Mfanyakzi wa Google akipata usingizi kwenye kitanda maalum kinachozuia mwanga na sauti ya kukoroma isisikike

  Mfanyakazi wa Google akimshika mbwa wake huku akiendelea na kazi zake


 Mfanyakazi wa Google akikatwa nywele kwenye Saluni ya ofisini

Post a Comment

 
Top