
Ubelgiji imejikita zaidi kileleni kwa kundi H, baada ya kuichakaza Estonia kwa magoli 8-1 katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya kombe la dunia uliofanyika Jijini Brussels.
Katika mchezo huo Dries Mertens na Romelu Lukaku walitumia wavuni magoli mawili kila mmoja, ambapo pia Thomas Meunier, Eden Hazard na Yannick Carrasco walifunga huku Ragnar Klavan akijifunga.
Hata hivyo mchezo huo umeiacha Chelesa na hofu ya kumkosa mchezaji wao Hazard, baada ya kutoka nje ya uwanja katika dakika ya 74, ikionekana kuwa ameumia goti.

Mshambuliaji Romelu Lukaku akijaribu kuwatoka mabeki wa Estonia

Eden Hazard akiwajibika katika mechi hiyo ambayo hata hivyo hakuweza kumaliza baada ya kuumia
Post a Comment