0


Mchezaji wa Manchester United, Memphis Depay, amefunga mara mbili wakati Uholanzi ikiifunga Luxembourg magoli 3-1 katika mchezo wa kuwania kufuzu kutinga michuano ya kombe la dunia 2018.

Depay, aliyesainiwa na Manchester United kwa paundi milioni 25 akitokea PSV mwaka 2015, amecheza dakika 20 akiwa na Manchester United katika Ligi Kuu ya Uingereza katika msimu huu.


Lakini akitokea benchi Depay alifunga goli lake la kwanza kwa mpira wa kichwa na kwa shuti la mpira wa adhabu, huku Arjen Robben akiwapa Wadachi hao goli la kuongoza lililozawazishwa na Maxime Chanot.
Arjen Robben akiachia shuti lililozaa goli la kwanza la Uholanzi
Memphis Depay akishangilia baada ya kufunga goli

Post a Comment

 
Top