
Timu ya Manchester United itakutana na mshambuliaji wake wa zamani Robin van Persie katika Kundi A la michuano ya Ligi ya Uropa.
Kikosi hicho cha Jose Mourinho kitakutana na mshambuliaji huyo Mdachi akiwa na Fenerbahce, pia kundi hilo zipo timu za Feyenoord na Zorya Luhansk ya Ukraine.
Kwa upande mwingine Southampton, imewekwa Kundi H, ikivaana na timu yenye fedha nyingi Inter Milan, Sparta Prague pamoja na Hapoel Be'er Sheva.

Manchester United na Inter Milan zinapewa nafasi kubwa ya kuwa ndio timu zitakazoshinda Ligi ya Uropa kwa mwaka huu.

Kwa upande mwingine Mtanzania Mbwana Samatta akiwa na Genk atakuwa na kibarua kigumu pale watakapovaana Athletic Bilbao, Rapid Vienna pamoja na Sassuolo katika Kundi F.
Post a Comment