0

 

Kiongozi wa Dubai Sheikh Mohammed bin Rashid amepatwa na mshangao baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za umma na kukutana na viti vitupu katika siku ya kazi huku maafisa waandamizi wa serikali wakiwa hawapo ofisini.

Sheikh Mohammed bin Rashid, alishangazwa na hali hiyo pale alipofanya ziara hiyo ya kushtukiza katika siku ya jumapili, alipokuwa akifanya ukaguzi siku hiyo ambayo ni siku ya kazi nchini Dubai.

Kufuatia hali hiyo ya uzembe mkubwa wa watumishi wa umma maafisa tisa waandamizi wa Manispaa ya Dubai wameagizwa kustaafu, baada ya ziara hiyo ya kushtukiza ya Sheikh Mohammed bin Rashid.
 

Post a Comment

 
Top