
David Rudisha amekuwa mwanariadha wa kwanza tangu Peter Snell wa New Zealand kutwaa mara mbili medali ya dhahabu katika mbio za mita 800 katika michuano ya Olimpiki mwaka 1964.
Rudisha raia wa Kenya aliongoza mbio hizo zikiwa katika umbali wa kilomita 300, baada ya Mkenya mwenzake Alfred Kipketer kuongoza katika mzunguko wa kwanza.
Katika mbio hizo Rudisha alimaliza kwa kutumia sekunde 42.15, mbele ya Taoufik Makhloufi wa Algeria na Mmarekani Clayton Murphy.
Post a Comment