
Baada ya kupita miezi miwili tangu machinjio ya nyama ya punda yaliyogharimu shilingi milioni 300 za Kenya kuanza kazi, bado hawajafanikiwa kusafirisha shehena ya kwanza ya nyama za punda kutokana na upatikanaji mdogo wa punda.
Waziri wa Kilimo Kenya Willy Bett alizindua machinjio hayo Aprili mosi mwaka huu, kwa lengo la kuuza nyama hizo za punda katika masoko ya China na Urusi pamoja Mashariki ya Mbali ambako nyama ya punda inahitajika sana.
Ili kufikia mahitaji ya soko hilo machinjio hayo yanahitaji kufikia mahitaji ya kusafirisha tani 100 hadi 200 za nyama ya punda katika mataifa hayo, ambapo kwa siku walipanga kuchinja punda 100.
Post a Comment