
Juan Jesus Gonzalez akiwa amepokelewa na aisa habari wa Azam FC Jafar Idd (Picha na Azam FC)
Jafar Idd Maganga amethibitisha ujio wa golikipa huyo mzungu ndani ya Azam FC kutoka bara la Ulaya.
“Leo tumempokea golikipa mmoja kutoka Hispania anaitwa Jesus Gonzalez, tumepokea mchana wa leo akitokea Hispania atakuwa ni miongoni mwa wachezaji wanaokuja kufanya majaribio kuelekea msimu ujao,” amesema Jafar Idd wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Spots ExtrA cha Clouds FM.
“Ilikuwa si rahisi kwa uongozi kuwaalika wachezaji au kuingia mkataba na wachezaji kabla ya mwalimu hajafika, mwalimu tayari amefika kwahiyo wachezaji wataalikwa kutoka nchi mbalimbali za Afrika, wale ambao ataona wanafaa watasajiliwa na Azam FC.”
Post a Comment