
Mmoja wa wanafunzi wakike waliotekwa huko Chibok nchini Nigeria amepatikana, ikiwa ni mwanafunzi wa kwanza kupatikana tangu miaka miwili kupita.
Mwanafunzi huyo Amina Ali Nkeki alikutwa jumanne akiwa amebeba mtoto na kundi la wapiganaji waliojitolea kujilinda akiwa kwenye Msitu wa Sambisa karibu na mpaka wa Cameroon.
Mwanafunzi huyo alikuwa namtu anayeshukiwa kuwa ni mmoja wa wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Wanafunzi wa kike 218 hawajulikani walipo baada ya kutekwa shuleni na Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria Aprili 2014.
Post a Comment