0













Leo ni siku ya maamuzi kwa Makocha wa Mataifa ya Ulaya kutangaza vikosi vyao vitakavyoshiriki michuano ya Mabingwa wa Ulaya, Euro 2016, kabla ya muda wa kufanya maamuzi hayo haujamalizika usiku.

Mataifa 24 yatashiriki michuano hiyo ya kipindi cha majira ya joto, yote yatalazimika kuthibitisha vikosi vyao vya wachezaji 23 mwisho ikiwa ni saa tano usiku, ambapo pia kibarua hicho pia wanacho makocha wa mataifa ya Uingereza, Wales na Jamhuri ya Ireland.


Kocha wa timu ya Uingereza almarufu kama Simba Watutu, Roy Hodgson, anahitaji kupunguza kikosi chake huku Fabian Delph akiwa imefahamika hatakuwemo, wakati wachezaji Ross Barkley, Andros Townsend, Danny Drinkwater na Marcus Rashford wakitarajiwa kuwamo.

Post a Comment

 
Top