0
Tume ya vyuo vikuu Tanzania TCU imevifuta vyuo vikuu vitatu chuo cha kilimo sayansi na teknolojia Mtakatifu Joseph Iringa, chuo kikuu kishiriki cha teknolojia ya Habari cha Songea na chuo kikuu kishiriki cha uongoziuhasibu na fedha mtakatifu Makambako kwa kushindwa kusimamia ubora na taaluma pamoja na ukiukwaji wa sharia ya kuendesha vyuo hivyo.
Taarifa zilizothibitishwa na millardayo.com ni kutoka kwa katibu mtendaji wa vyuo vikuu Tanzania Profesa Yunus Mgaya aliyenukuliwa akisema > Kama unafundisha Teknolojia ya uhandisi, shahada ya uhandisi wa kilimo tunategemea Wanafunzi wako wawe ni Wahandisi wanaoweza kuendesha Trekta ikiwa ni pamoja na kulitengeneza pamoja na vitu vyote vya kihandisi kwenye kilimo
‘Tukija kwenye chuo chako na tukikosa vitu hivyo na pale tumekuta vipo kwenye viwango vya chini sana tukaona kwamba hawa Wanafunzi hawatotoka hapa wakiwa wanaulinganifu hata wa karibu na wenzao wanaosoma Sokoine’ – Profesa Mgaya.

Post a Comment

 
Top