0

                                Hifadhi ya Msitu
Juhudi kubwa ya kufikisha elimu kwa jamii juu ya uhifadhi, usimamizi na uvunaji endelevu wa misitu iliyofanywa na serikali kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali kupitia kampeni mbalimbali ikiwemo ya mama misitu inayofadhiliwa na nchi ya Finland imeanza kuzaa matunda.

Baada vijiji kuanza kuhifadhi misitu, na wananchi kuunga mkono juhudi hizo baada yakuanza kunufaika na utunzaji huo.

Miongoni mwa vijiji ambavyo wananchi wake wameanza kunufaika na uhifadhi wa misitu ni kijiji cha Nanjirinji A, kilichopo wilayani Kilwa mkoani Lindi.

Wananchi wa kijiji hicho wameanza kunufaika na mpango huo kupitia mapato ya uvunaji wa mazao ya msitu wao wa Mbumbila.

Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji hicho, Jafariri Nyambate alisema wameanza kutoa ruzuku kwa akinamama wajawazito wakazi wa kijiji hicho. Kila mjamzito hupewa shilingi 30,000 anapokaribia muda wake wakujifungua. Alisema.

Alisema hilo nijambo moja kati ya mengi yaliyofanywa na kijiji hicho kwa wananchi kutokana na mapato ya msitu waliohifadhi unaojulikanakwa jina la Mbumbila.

Nyambate ambaye kijiji chake pia kimeweza kuwanunulia sare wanafunzi wa shule ya msingi ya kijiji hicho, kuchimba visima vya maji, kujenga soko la kijiji, madarasa, nyumba ya mwalimu, kuweka umeme jua kwenye shule ya kijiji hicho na kutoa ruzuku kwa akinamama wajawazito, alisema uenda mafanikio hayo yasiwe endelevu.

Kutokana na uvamizi wa wakulima na wavunaji haramu unatishia kurudisha nyuma mafanikio hayo, kwani juhudi zakuwaondoa zimekuwa ngumu kufanikiwa kwasababu wakulima wamekuwa wakirejea kila unapofika msimu wa kilimo wa zao la ufuta.

"Wanatumia nguvu kulima ndani ya msitu na wanapambana na kamati yetu ya maliasili inapofanya doria, mara moja wamewahi kuwazidi nguvu walinzi wetu na kupora pikipiki," alisema Nyambate.

Kuhusu uvunaji haramu, Nyambate alisema wakulima na wavunaji haramu wengi wanatoka nje yakijiji na wilaya hiyo, akibainisha kwamba kuna mahusiano na ushirikiano mkubwa kati ya wakulima wavamizi na wavunaji haramu.

"Wakulima wengi wanaishi kwenye misitu ya hifadhi ya wazi ambayo inapakana na msitu wetu, wanawaongoza wavunaji haramu ambao mazao ya msitu wanayoiba wanahifadhi ndani ya vibanda vya wakulima hao,"alisema Nyambate.

Ofisa mtendaji kata wa kata ya Nanjirinji, Haji Limba, alikiri kuwa mapato yanayotokana na msitu huo yamesababisha kuanza kuwa na uhakika wa ulinzi kwenye kata hiyo iwapo ujenzi wa kituo cha polisi kinachojengwa katika kata hiyo kitakamilika.

Alisema sehemu ya fedha zinazotumika katika ujenzi huo zilichangwa na kijiji hicho ambazo zilitokana na mauzo ya mazao ya msitu wa kijiji hicho.

Hata hivyo alibainisha kwamba wakulima wa ufuta na wavunaji haramu wnatishia kukwamisha mafanikio yaliyoanza kufikiwa.

"Hata hivyo juhudi kubwa inayofanywa na uongozi wa kijiji,kata,halmashauri ya wilaya na mkuu wa wilaya ya Kilwa zinapunguza kasi ya uvamizi wa wakulima hao na wavunaji haramu,maana msaada kutoka wilayani ni mkubwa sana,"alisema Limba.

Naye mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Ngunichile wilayani Nachingwea, Seif Ng'wang'wa ambaye kijiji cha kimehifadhi msitu wenye ukubwa wa hekta 1296 unaojulikana kwa jina la Namitonga, alisema wavunaji haramu baada ya kumaliza miti katika misitu ya wazi ya vijiji jirani na kijiji hicho, wameanza kuvamia msitu huo.

Alisema kazi ya kuulinda imekuwa ngumu baada ya wavamizi kubadili mbinu.

"Tunajitahidi sana kufanya doria mchana, walipogundua kuwa mchana inawawia vigumu kufanya uhalifu wanafanya usiku,"Alibainisha kuwa uharibifu unaofanywa na wavunaji haramu unatishia kufikiwa na kutekelezwa mipango ya maendeleo ambayo utekelezaji wake ulitegemea mapato ya mauzo ya mazao ya msitu huo.

Ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Seleman Soya alisema licha ya wavunaji haramu lakini pia changamoto nyingine niwakulima kuvamia msitu huo.

"wavamizi niwengi nivugumu sisi wenyewe kukabiliana nao, watatushinda nguvu inahitajika nguvu kubwa kutoka serikalini vinginevyo watazidi kuumega,"alisema na kutahadharisha Soya.

Alisema migogoro ya mipaka baina ya vijiji hasa ambavyo havija hifadhi misitu inachangia kukwamisha wananchi kukosa matumaini ya kunufaika na msitu huo.

Bibi Arafa Batazari(80) mwananchi wa kijiji hicho, alisema licha ya wananchi kutarajia kunufaika na mauzo ya mazao ya msitu huo, lakini pia hali ya ukame inaweza kurejea katika maeneo hayo.

Post a Comment

 
Top