
Muwania urais wa Marekani Bw. Donald Trump amekejeliwa na wagombea wenzake wa chama cha Republican katika mdahalo uliorushwa kwenye Televisheni kutokana na mgogoro wake na kituo cha Fox News.
Mgombea huyo machachari aliamua kujitoa kwenye mdahalo huo kutokana kituo hicho kukataa kumuondoa mtangazaji Megyn Kelly kuongoza mdahalo, ambaye Bw. Trump anamtuhumu kwa kuwa na upendeleo.
Badala yake bilionea Bw. Trump aliitisha mkutano wa hadhara karibu na mdahalo huo kwa ajili ya kuwaenzi mavetenari wa vita, jambo ambalo lilitishia kuathria idadi ya watu iliyofuatilia mdahalo huo.
Jumatatu ya wiki ijayo huko Iowa, wapigakura wanatapiga kura kuwateuwa mgombea wao wa urais wa vyama vyao.
Post a Comment