0


















Kundi la mawakili, wanaharakati na wanasayansi nchini Brazil wameiomba mahakama kuu ya nchi hiyo kuruhusu utoaji kwa wanawake wenye virusi vya Zika.

Virusi vya Zika vinavyoonezwa na mbu vimekuwa vikihusishwa na kuzaliwa watoto wenye vichwa vidogo na ubungo usiokomaa.

Utoaji mimba ni kinyume na sheria za Brazil, isipokuwa pale kwa dharura za kiafya ama mimba iliyotokana na kubakwa.


Watu milioni tatu hadi milioni nne wanaweza kuathiriwa na virusi vya Zika katika mataifa ya amerika mwaka huu.

Post a Comment

 
Top