0


Ligi kuu soka nchini England maarufu kama Barclays Premier League imefikia zaidi ya nusu msimu wikendi hii na kushuhudia klabu ya soka ya Arsenal ikisalia kileleni mwa ligi hiyo na kuwaacha Leicester City na Manchester City katika nafasi za pili na tatu katika msimamo.
Arsenal inapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo msimu huu ambapo mara ya mwisho ilikua ni msimu wa 2003/04 walipotwaa bila kupoteza mchezo, na hizi ndio sababu zinazoipa nafasi Arsenal kutwaa ubingwa;
  1. Magoli ya Oliver Giroud
Kwa takribani misimu miwili sasa klabu ya Arsenal imekua ikikwamishwa na uwezo hafifu wa mshambuliaji wao (Oliver Giroud) kufunga magoli mengi na muhimu ili kuisaidia timu yao kukusanya points za kutosha kushinda ubingwa.
Msimu huu tangu kocha wake aanze kumtumia Theo Walcott kama mshambuliaji wa kati na kumuacha nje Giroud, kulimfanya mshambuliaji huyo aamke na kuanza kufunga kila apatapo nafasi ya kupangwa.
  1. Kuikidhi hali ya majeruhi
Majeruhi umekua ni ugonjwa mkubwa katika kikosi hiki cha kocha Arsene Wenger kwa misimu kadhaa sasa. Katika misimu kadhaa iliyopita tumekua tukishuhudia namna Arsenal walivyokua wakihangaika na kuanza kupoteza michezo kutokana na kuumia kwa baadhi ya wachezaji wao muhimu.
Lakini msimu huu pamoja na idadi kubwa ya majeruhi ya akina Jack Wilshere, Danny Welbeck, Alexis Sanchez, Saint Carzola, Thomas Rosiscky na Qoqueline lakini bado wamesimama imara na wameshinda takribani mechi zote.
  1. Msimu dhaifu wa ligi
Kwa vyovyote vile, mtakubaliana nami kuwa huu ni msimu dhaifu zaidi kushuhudia katika ligi kuu soka nchini England. Arsenal wanaweza pata faida kubwa ya kutwaa ubingwa kutokana na ushindani hafifu kutoka kwa miamba wa ligi hii (Manchester United, Chelsea) kutokua na msimu mzuri, huku pia vilabu vya Liverpool na Manchester City vikionekana kuwa na homa za vipindi.
Leicester City ambao wamekua na msimu mzuri zaidi hivi sasa, siwapi nafasi kubwa sana kutokana na sababu za ukubwa wa kikosi chao na uzoefu.
  1. Uzoefu wa Petr Cech katika ulinzi
Safu ya ulinzi ya klabu ya Arsenal imekua ikifanya makosa mengi sana katika misimu kadhaa iliyopita kutokana na kukosa uongozi katika safu hiyo.
Kuongezeka kwa golikipa Petr Cech kutoka Chelsea msimu huu kumeongeza kitu cha ziada kutokana na uwezo wake mkubwa wa kushinda mechi na kujua kuwapanga walinzi wake vizuri. Arsenal sasa haifungwi magoli mengi ya kizembe kama ilivyokua hapo nyuma.
  1. Kiu ya ubingwa
Pamoja na mambo mengine yote niliyoyasema, lakini pia Arsenal wasingekua hapo walipofika kama wasingekua na kiu na ubingwa huo ambao mara ya mwisho klabu hiyo ilitwaa misimu 11 iliyopita

Post a Comment

 
Top