0


Mchezo wa kwanza wa kocha Pep Guardiola wa FA umemalizikia kwa ushindi mnono baada ya Manchester City kuichakaza West Ham kwa magoli 5-0 katika mchezo wa raundi ya tatu.

Manchester City ilikuwa inaongoza kwa magoli 3-0 hadi mapumziko ambapo Yaya Toure alifungua mvua ya magoli kwa shuti la mpira wa penati.

Havard Nordtveit alitumbukiza kimakosa mpira kwenye wavu wao kufuatia krosi ya Bacary Sagna, katika sekunde ya 146 kabla ya David Silva kufunga la tatu.

Muda mfupi baada ya kuanza kipindi cha pili Sergio Aguero aliunganisha wavuni mpira uliopigwa na Toure na kisha John Stones kufunga la tano.
 Mpira wa penati uliopigwa na Yaya Toure ukijaa wavuni

Post a Comment

 
Top