0


Mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane, amefunga goli wakati Senegal ikiifunga Zimbabwe na kuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika 2017.

Katika mchezo huo Sadio Mane alifunga goli la kwanza kwa shuti la karibu katika dakika ya tisa akiunganisha pasi ya mchezaji wa Lazio, Keita Balde Diao.

Mchezaji Henri Saivet, anayecheza kwa mkopo St Etienne akitokea Newcastle, alifunga goli zuri la pili kwa shuti la yadi 20, dakika nne tu kupita tangu kufungwa goli la kwanza.
Katika mchezo wa awali hapo jana Tunisia imejiweka katika nafasi nzri ya kusonga robo fainali ya michuano hiyo baada ya kuwafunga majirani zao Algeria magoli 2-1.

Post a Comment

 
Top