0


Wafungwa wapatao 33 wameuwawa katika gereza kaskazini mwa Brazil, ikiwa ni siku chache tu kupita tangu wafungwa 56 kufa wakati wa ghasi zilizotokea kwenye gereza la jimbo jirani.

Miili 30 imekutwa ikiwa imetenganishwa vichwa vyao na viwiliwili maafisa wa gereza hilo la Brazili wamesema.

Waziri wa Sheria wa jimbo hilo Uziel Castro amelishutumu kundi la dawa za kulevya la Roraima kwa kuhusika na mauaji hayo.

Hata hivyo hali katika gereza hilo la Monte Cristo lenye mrundikano wa wafungwa imerejea katika hali ya utulivu.

Post a Comment

 
Top