0
Wanafunzi katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha (AJTC) kutoka katika darasa la Mt.Kilimanjaro lilipo chuoni hapo  jana walitembelea kituo cha kulele a watoto yatima na wasio jiweza cha Karim Chldern Care Centre kilichopo eneo la Morombo jiji Arusha.

Wanafunzi hao walitembelea kituo hicho wakitekeleza kwa vitendo somo la (Public relation) kwa kufikia jamii moja kwa moja hasa kwa makundi yasio jiweza ikiwa ni moja ya mafunzo wanayo pata chuoni hapo.



Mkuu wa chuo cha Arusha Jornalism Traing College (AJTC) na kufunzi wa somo la Public relation BW.Andrea Ngobole akihimiza wanafunzi kupanda kwenye gari tayari kuelekea katika kituo hicho. 


Wanafunzi wakiingia katika gari ilikuondoka kuelekea katika kituo cha kulelea watoto wanaolelewa katika kituo cha Karim Children Care Centre.

Wanafunzi hao wakiwa kwenye gari tayari kuelekea katika kituo hicho

Wanafunzi hao wakiwa wamewasili katika eneo hilo huku huku Bw.Ngobole akiteta jambo na wanafunzi hao 

Bw.Ngobole akiongoza wanafunzihao kuingia katika kituo hicho bara baada yakuwasili eneo hilo.

Wanafunzi kutoka katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha (AJTC) wakiendelea kuingia katika kituo hicho.

Wanafunzi hao wakivua viatu tayari kuingia ndani ya yumba hiyo wanapolelewa watoto hao.

Mlezi wa kituo hicho akiteta jambo baada ya wanafunzi hao  kuwasili  katika kituo hicho kilichopo eneo la kwa morombo (dampo)

Wanahabari wakifanya kazi yao wakati malezi huyo alipokuwa akielezea mambo mbali mbali wanayokabiliana nayo huku moja ya mabo aliyo yazungumzia ni kutokuwa na huduma ya umeme katika kituo hicho na kuwaomba wasamariawema kumsaidia,ili watoto hao waweze kujisomeanyakati za jioni mwanaporejea kutoka shuleni. 

Wanafunzi hao wakifuatilia kwa umakini.


Mlezi huyo wa Karim Children Carecentre akiteta na wanafunzi hao wakati alipokuwa anawaonyesha mazingira na vyumba wanavyo vitumia watoto hao.



Wanafunzi hao wakishiriki kazi mbalimbali ndani ya kituo hicho. 

Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Kaim Children Carecentre. 

Bi.Gretude Mpenzie ambae ni mwanafunzi katikachuo cha (AJTC) akikabidhi mafuta kwa watoto hao ikiwa ni moja ya vitu walivyo waletea watoto hao.

Bi.Kamile Issaya akikabithi mche wa sabuni kwa watoto hao ilikuwasidia katika shughuli za ufuaji wa nguo zao. 

Bi.Neema Temu akiwakabidhi mchele watoto hao ikiwa nimoja ya vitu walivyo toa kwa watoto hao wa kituo cha Karim Children Carecentre kilichopo eneo la Morombo jijini Arusha.

Makamu wa Rais katika chuo cha (AJTC) Bi.Judith Urio akitoa zawadi kwa watoto hao.

Mlezi wa kituo hicho akitoa neno la shukrani mara baada ya kuwakabidhi watoto hao vitu mbalimbali.
Wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo hicho




Wanafunzi hao wakirejea Chuoni bara baada ya kufanikisha kwa ustadi wa hali ya juu kile walicho kitarajia ndani ya ktuo cha kulelea watoto yatima na wale waishio katika wazingira magumu cha Karim Children Carecentre.

PICHA ZOTE NA SAMWELY WILSON

Post a Comment

 
Top