
Maelfu ya waandamanaji wameingia mitaani katika miji kadhaa ya Marekani kupinga ushindi wa urais wa Donald Trump.
Watu hao wengi wao wamekuwa wakipaza sauti wakisema “Trump sio rais wangu” na wengine wakichoma moto masanamu ya mfanyabiashara huyo aliyeshinda urais.
Trump atakuwa rais wa 45 wa Marekani baada ya kupata ushindi wa kushtukiza dhidi ya mgombea wa Democratic, Bi. Hillary Clinton.

Waandamanaji wakiwa na mabango huku sanamu ya Donald Trump ikiwa imening'inizwa juu

Waandamanaji wakichoma moto bendera ya Marekani

Maandamano hayo pia yaliambatana na vitendo vya kuchomwa magari
Post a Comment