
Mchezaji wa zamani wa Ujerumani Kocha Jurgen Klinsmann amefukuzwa kuinoa timu ya taifa ya Marekani.
Klinsmann, 52, ambaye alishinda kombe la dunia na Ujerumani mwaka 1990, alikuwa akiinoa Marekani tangu mwaka 2011.
Uamuzi wa kumtosa Klinsmann umekuja baada ya Marekani kupoteza nyumbani 2-1 dhidi ya Mexico na kufungwa ugenini 4-0 na Costa Rica katika michezo wa kuwania kufuzu kombe la dunia.
Post a Comment