
Timu ya Real Madrid imeishushia kipigo cha paka mwizi timu ndogo ya daraja la tatu ya Cultural Leonesa kwa kuichakaza kwa magoli 7-1 katika mchezo wa kombe la Copa del Rey.
Katika mchezo huo ambao Madrid waliwapumzisha Cristiano Ronaldo, Gareth Bale na Karim Benzema, walipata goli la kwanza baada ya mchezaji wa zamani wa West Brom beki Gianni Zuiverloon, kujifunga
Magoli mengine ya Real Madrid yalifungwa na Marco Asensio na Alvaro Morata waliofunga magoli mawili na Nacho na Mariano walifunga moja kila mmoja.

Gianni Zuiverloon akiwa amempoteza mahesabu kipa wake na kujifunga

Marco Asensio akifunga goli la pili la Real Madrid
Post a Comment