
Mwanamuziki maarufu wa Jazz nchini Kenya, ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa kwenye Tusker Project Fame, Achieng Abura amefariki dunia jana katika hospitali ya Taifa ya Kenyatta (KNH).
Abura alikuwa amelazwa kwenye wodi ya binafsi katika hospitali hiyo tangu Oktoba 13, akipatiwa matibabu ya ugonjwa ambao haujaelezwa.
Mapema mwezi huu mwanamuziki huyo alitumia mitandao ya jamii, kueleza kuwa hali yake ya kiafya sio nzuri na madaktari walimshauri aongeze uzito na kisha apunguze kupitia mazoezi.
Post a Comment