
Mfalme wa Morocco Mhe. Mohammed VI ( wa mbele) akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara rasmi ya siku tatu Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Mfalme wa Morocco Mohammed VI akipokea shada la maua

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Mfalme wa Morocco Mohammed VI mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Mfalme wa Morocco Mohammed VI wakisimama kwa nyimbo za Taifa.

Mfalme wa Morocco Mohammed VI akikagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili nchini.
Post a Comment