
Baada ya kutwaa taji la EPL msimu uliopita, Leicester wanapita katika kipindi kigumu kwa sasa kwenye ligi hiyo inayofatiliwa na mashabiki lukuki wa soka duniani.
Mabingwa hao watetezi wa Premier League wanaonekana hakuna wanachokifanya kwenye ligi ya nyumbani kwao .
Wameshapoteza michezo dhidi ya Chelsea, Liverpool, Manchester United na kwa uhalisia wanataraji kumaliza msimu wa ligi kwa heshima angalau katika nafasi za katikati ya msimamo kati ya timu 20.
Lakini kwa upande wa Champions League ni habari nyingine kabisa, walifuzu kwa mara ya kwanza bada ya kutwaa taji la ligi msimu uliopita.
Kwa ushindi wa walioupata dhidi ya FC Copenhagen usiku wa Jumanne October 18, tayari wamejihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya 16 bora, pointi 10 zinatosha kujihakikishia kufuzu na wao hadi sasa wameshafikisha pointi 9 wakiwa wamebakiza mechi tatu katika hatua ya makundi.
Pointi nyingi UEFA Champions League kuliko Premier League
Wana pointi nyingi kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya (9) kuliko zile walizonazo Premier Lague (8).
Wameshacheza mechi 8 za Premier League, wakati huo wamecheza mechi tatu upande wa mechi za mashindano ya Ulaya.
Kila mmoja anaweza kufukiri kwamba, wanajaribu kuwekeza kuvu zao kwenye mashindano ya Ulaya msimu huu kuliko Premier League.
Matokeo yote ya mechi za UEFA Champions League Jumanne October 18, 2016

Post a Comment