Zlatan Ibrahimovic amefunga goli katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza wakati Manchester United ikiibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Bournemouth na kumpatia kocha wao mpya Jose Morinho ushindi wa kwanza.
Katika mchezo huo Juan Mata alikuwa wa kwanza kuifungia Manchester United katika dakika ya 40 kufuatia makosa yaliyofanywa na mabeki wa Bournemouth, ambapo baadaye katika dakika ya 59 Wayne Rooney alifunga la pili kwa mpira wa kichwa.

Juan Mata akifunga goli la kwanza la Manchester United baada ya mabeki kufanya uzembe

Mchezaji mpya wa Manchester United Eric Bailly akituliza mpira gambani huku akiwa ameruka juu

Post a Comment