0

 

Serikali ya Bolovia imesema naibu waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo ametekwa na kuuwawa na wachimba madini waliokuwa kwenye mgomo.

Waziri huyo Rodolfo Illanes na mlinzi wake walitekwa siku ya Alhamisi kwenye kizuizi cha barabarani eneo la Panduro, kusini mwa La Paz.

Waziri wa Mambo ya Ndani Carlos Romero amesema kuna kila dalili kuwa Bw. Illanes ameuwawa kwa kushambuliwa kikatili.

Wachimbaji madini wawili nao wamekufa kwa majeraha ya risasi baada ya kupambana na polisi.

Post a Comment

 
Top