
Mwanasoka shujaa wa Brazil katika mchezo wa soka katika michuano ya Olimpiki, Neymar ameonekana akishangilia timu ya mpira wa wavu ya wanaume ya Brazil katika mchezo wa fainali ambao walishinda medali ya dhahabu.
Neymar, ambaye amejivua wadhifa wa Kapteni wa Brazil, alifunga penati ya ushindi dhidi ya Ujerumani na kusaidia Brazil kutwaa medali ya dhahabu pamoja na kulipa kisasi cha kufungwa na Ujerumani katika mchezo wa nusu fainali za kombe la dunia.
Timu ya mpira wa wavu ya Brazil iliishinda Italia jana na kutwaa medali ya dhahabu na kuchangia kuweka rekodi bora ya Brazil katika michuano hiyo kwa kutwaa medali saba za dhahabu katika michuano hiyo ya Rio 2016.

Post a Comment