
Rio imemaliza michuano ya Olimpiki kwa shamrashamra za aina yake, licha ya mvua kuwanyeshea maelfu wanamichezo pamoja na watazamaji waliofika kushuhudia michezo hiyo kutoka maeneo mbalimbali duniani.
Mwenge wa Olimpiki umezimwa katika uwanja wa Maracana nchini Brazil, na kuashiria michuano ya Olimpiki Rio imemalizika rasmi.
Gavana mpya wa Tokyo, Yuriko Koike, ambaye ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo alipokea bendera ya Olimpiki kutoka kwa Meya wa Rio, Eduardo Paes, ikiwa ni kuipokeza Japan jukumu la kuandaa michuano ijayo ya Olimpiki.



Watumbuizaji wakitumbuiza kwa furaha wakati wa sherehe za kufungwa michuano ya Olimpiki Rio 2016

Post a Comment