0


Kocha Pep Guardiola atarejea Barcelona akiwa na Manchester City baada ya klabu yake hiyo mpya kupangiwa kukutana na Barcelona katika droo ya Ligi ya Mabigwa Ulaya.

Guardiola ambaye alishinda mara mbili kombe la michuano hiyo akiwa na Barcelona, aliiongoza City kufuzu kuwania kutinga katika michuano hiyo kwa kuifunga Steaua Bucharest.

Timu hizo zipo katika kundi la C, wakiwa pamoja na Borussia Monchengladbach na Scottish champions Celtic.

MAKUNDI YOTE YA UEFA YAMEPANGWA KAMA IFUATAVYO:-
KUNDI A: Paris Saint-Germain, Arsenal, Basle na Ludogorets, KUNDI B: Benfica, Napoli, Dynamo Kyiv na Besiktas, KUNDI C: Barcelona, Manchester City, Borussia Monchengladbach na Celtic, KUNDI D: Bayern Munich, Atletico Madrid, PSV Eindhoven na Rostov.
Aidha, katika hafla hiyo UEFA imemtangaza mshambuliaji nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo kuwa mwanasoka bora wa UEFA.

Post a Comment

 
Top