0


Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akigonganisha bilauri na Mke wa Rais wa Rwanda, Mama Jeannette Kagame katika kusherehekea Dhifa ya Kitaifa aliyomuandalia mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame (katikati) Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais Kagame alikuwa nchini kwa ziara ya Kikazi.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kulia) akigonganisha bilauri na Rais wa Rwanda Paul Kagame, katika kusherehekea Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya mgeni wake Rais Kagame. Dhifa hiyo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akifurahia jambo na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame.


 Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa tatu kushoto) akiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim (wa pili kushoto), Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman (wa tatu kulia) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo (kulia).

Post a Comment

 
Top