0


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir Mhe,Mohamed Raza Daramsi wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akifuatana na Viongozi na Mashekhe wa jumuiya hiyo kwa ajili ya kukabidhi msaada wa madawati 100 kwa ushirikiano na familia ya Rais wa Jumuiya,msaada huo utaowanufaisha wanafunzi wa Skuli mbali mbali za Zanzibar

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma akitoa shukurani kwa Uongozi wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir wakati ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kukabidhi madawati 100 kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) ikiwa ni katika kuimarisha sekta ya Elimu hapa Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia)akikabidhiwa madawati 100 kutoka kwa Viongozi wa jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir na familia ya Rais wa Jumuiya hiyo Mohamed Raza walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,msaada huo kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar, 02/07/2016.[Picha na Ikulu.]

Post a Comment

 
Top