
Nchi ya Niger imesema miili ya wahamiaji 34 wakiwemo watoto 20 imekutwa katika jangwa la Sahara karibu na mpaka wa Algeria.
Taarifa ya serikali ya Niger imesema miili hiyo imekutwa karibu na mji mdogo wa Assamakka.
Waziri wa Mambo ya Ndani Bazoum Mohammed amesema wahamiaji hao inaonekana wamekufa kutokana na kiu, baada kutelekezwa jangwani na wasafirishaji binadamu.
Post a Comment