
Mabasi mengi ya abiria nchini Kenya maarufu kama Matatu katika Jiji la Nairobi yana kunguni hali ambayo inatatiza biashara ya usafiri katika Jiji hilo Kuu la Kenya.
Wadudu hao wanaonyonya damu sasa wanatishia kuathiri biashara ya usafirishaji abiria Jijini Nairobi, kutokana na watu wengi kuhofia huduma za mabasi hayo.
Kunguni hao wamekuwa wakilitwa kwenyea mabasi na abiria bila ya kufahamu kutokea nyumbani kwaona kuishia kwenye viti.
Kwa sasa watoaji usafiri huo wa umma wameanza kampeni ya kukabiliana na kunguni kwa kunyunyuzia dawa na kuwataka abiria kuwasilisha malalamiko yao iwapo wataona kunguni kwenye Matatu.

Post a Comment