
Wachezaji na viongozi wa timu ya taifa ya Uganda
wanataka kumuenzi golikipa wao Dhaira kwa
kuhakikisha wanafuzu kwenye fainali za Africa Cup
of Nations mwaka 2017 ambazo zitafanyika Gabon.
Shughuli za mazishi zimefanyika Jumatatu kwenye
jiji la Kampala, Dhaira, 28, alifariki juma lililopita
akiwa nchini Iceland kutokana na ugonjwa wa
cancer
Tutapambana sana kuhakikisha tunafuzu kwenye
fainali zitakazofanyika Gabon kwa ajili ya heshima
ya Dhaira”, Moses Magogo ambaye ni rais wa FA
ya Uganda aliiambia BBC.
Uganda kwa sasa ipo kundi D ikiwa na pointi 7
sawa na Burkina Faso huku timu hizo zikiwa
zimelingana kwa kila kitu kwenye kundi hilo lakini
Burkina Faso inakaa kileleni mwa kundi kulingana
na mpangilio wa ‘alphabet’.
Tonny Mawejje ambaye ni mchezaji mwenzake na
Dhaira kwenye timu ya taifa pia akiwa amewahi
kucheza Iceland ameunga mkono kauli iliyotolewa
na Magogo.
“Ni vigumu kuzungumzia mchezo wa mpira wa
miguu halafu usilitaje jina la Dhaira, alikuwa
anamchango mkubwa kwenye nchi hii”, Magogo
aliendelea kusema.
Kocha wa sasa wa Uganda Milutin Sredojevic
‘Micho’ pia amemzungumzia golikipa huyo ambaye
aliwahi kucheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania
bara akiwa na klabu ya Simba SC.
“Abel was a close friend to many of the Uganda
Cranes players we are devasteted by his
unexpected passing,” he explained.
“Abel alikuwa ni rafiki wa wachezaji wengi wa
Uganda Cranes kifo chake kisichotarajiwa
kimetuachia machungu ,” amesema.
Tunapoelekea michezo yetu miwili ya mwisho ya
kufuzu Mataifa ya Afrika, tutakuwa na sababu
kubwa ya kufuzu kwenye fainali hizo baada ya
miaka 39 kwa ajili ya Abel Dhaira”.
“Uganda imepoteza golikipa muhimu na siku zote
tutaendelea kumkumbuka”
Dhaira atazikwa leo (Jumanne) kwenye wilaya ya
Mayuge, Mashariki mwa Uganda.
Alicheza mchezo wake wa kwanza kwenye timu ya
taifa mwaka 2009 na kuisaidia The Cranes kutwaa
ubingwa wa CECAFA Senior Challenge Cup mwaka
2012 mashindano yaliyofanyika kwenye ardhi ya
Uganda.
Licha ya kucheza nchini Iceland, enzi za uhai wake
aliwahi kuvitumika vilau kadhaa kama Express na
URA za Uganda, kisha akaelekea AS Vita ya DR
Congo na baadaye Simba SC ya Tanzania.
Inaelezwa kuwa, mchezaji mwingine wa zamani
wa Uganda Mathias Kaweesa anapambana na
ugonjwa wa cancer.
Post a Comment