
HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA
TAARIFA KWA UMMA
Mnamo tarehe 01.04.2016 ilisambazwa taarifa ya uongo kwenye mitandao ya Kijamii ambayo kwa kiasi kikubwa ilipotosha Umma wa Watanzania kwamba kuna Kikao cha Baraza la Madiwani kilichokua kifanyike Tarehe 01.04.2016 kimevunjika na kuahirishwa hadi wiki ijayo kufuatia Waheshimiwa Madiwani kutoa hoja ya kutojadiliwa kwa Kabrasha mpaka hapo hoja mbili za nyuma zitakapojibiwa.
Tungependa wananchi waelewe kwamba taarifa hiyo si sahihi na inapotosha umma. Halmashauri ya Jiji la Arusha kama ilivyo Mamlaka zingine za Serikali za Mitaa Nchini inaendeshwa kwa Mujibu wa Sheria na Kanuni za uendeshaji wa shughuli za Serikali za Mitaa na Taratibu za uendeshaji wa vikao vya Halmashauri. Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya Halmashauti ya Jiji la Arusha kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani kilifanyika Feb 10, 2016 na kitaketi tena baada ya miezi mitatu.
Hii ina maana kwamba hakuna Kikao chochote kilichokua kifanyike Tarehe 01.04.2016 na wala hoja zilizotajwa kwenye taarifa hiyo si za kweli. Vikao vyote vya Baraza la Madiwani hutangazwa na Mkurugenzi wa Jiji kupitia vyombo vya Habari na viko wazi kwa Umma na mwananchi yoyote anaruhusiwa kuhudhuria.
Inawezeakana mtoa taarifa hizo pengine alikusudia kutumia tarehe 01 April kuwa siku ya wajinga lakini hakupaswa kutoa uongo kwa Umma katika maswala ambayo upotoshaji wake utaathiri jamii.
Napenda kuwaarifu watanzania wote kuipuuzia habari hiyo kwani haina ukweli wowote.
IMETOLEWA NA:
AFISA HABARI
Kny: MKURUGENZI WA JIJI
ARUSHA
02.04.2016
Post a Comment