0
Azam-mazoezi 8

Kikosi cha Azam FC leo April 29 asubuhi kimefanya mazoezi ikiwa ni maandalizi kuelekea pambano la Jumapili dhidi ya ‘Mnyama’ Simba SC mechi inayotarajia kutoa taswira ya timu moja kati ya hizo kuendelea kupambana na Yanga kuwania ubingwa wa VPL 2015-16.
Azam-mazoezi 4
Azam imefanya mazoezi kwenye uwanja wake wa nyasi za asili kutokana na mchezo wa Jumapili kuchezwa kwenye uwanja wa taifa ambao nyasi zake ni za asili.
Azam-mazoezi 5
Simba tayari imerejea jana kutoka Zanzibar ambako iliweka kambi ya kujiandaa kwa ajili ya mchezo huo wa Jumapili jioni.
Azam-mazoezi 3
Mchezo huo una maana kubwa kwa timu zote mbili kutokana na umuhimu wake, timu itakayoshinda mchezo huo itakua na matumaini makubwa ya kupambana na Yanga inayoongoza ligi ikiwa na pointi 62 ikifuatiwa na Azam yenye pointi 58 wakati Simba inapointi zake 57 huku timu zote tatu zikiwa zimecheza mechi 25 nq kusaliwa ma mechi tano tu.
Azam-mazoezi 6

Post a Comment

 
Top